9 Aprili 2015 - 19:36
Mazungumzo kuhusu Ukraine

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank - Walter Steinmeier amewaalika mawaziri wenzake kutoka Urusi

Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani  Frank - Walter Steinmeier  amewaalika  mawaziri  wenzake   kutoka  Urusi, Ukraine na  Ufaransa  mjini  Berlin  siku  ya  Jumatatu  kujadili utekelezaji  wa makubaliano  ya  amani  yaliyofikiwa  mjini  Minsk  kuhusu  mashariki mwa  Ukraine, nchini  Belarus Februari mwaka  huu.

Mzozo  kati  ya  waasi  wanaoungwa  mkono  na  Urusi  na  majeshi ya  serikali  ya  Ukraine  mashariki  mwa  nchi  hiyo  umesababisha watu 6,000  kupoteza  maisha.

Viongozi  wa  Ujerumani na  Ufaransa  wamesimamia  upatikanaji  wa makubaliano  ya  kusitisha  mapigano  mjini  Minsk  katika  juhudi  za kusitisha  umwagikaji  wa  damu , na  uhasama  umepungua  licha  ya kuwa  tofauti  bado  zipo katika  kupiga  hatua.

Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ufaransa  Laurent Fabius anaamini  kwamba  hatua  kiasi  za  maendeleo zimefikiwa  ndani  ya eneo  hilo  la  vita  licha  ya  ukiukaji  wa  makubaliano  ya  kusitisha mapigano.

Tukio  hilo  lililochukua  muda  wa  masaa 16  lilimalizika  wakati washambuliaji  wanne  wameuwawa  ama  kujiripua. Zaidi  ya  watu 100  wamejeruhiwa  katika  shambulio  hilo. Wizara  ya  elimu imekana  ripoti  kuwa  wanafunzi  166 bado  hawajulikani  waliko.